Marais wa EAC kuujadili mzozo wa mashariki mwa Kongo
27 Januari 2025Katika taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya Rwanda imesema ililazimika kujihami huku Balozi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa Ernest Rwamucyo akisema, haya ni matokeo ya kushindwa kwa utawala wa Kongo kushughulikia tatizo hilo.
" Hali tunayokabiliana nayo leo, haimshangazi mtu yeyote. Inaakisi hali iliyotokea miaka 12 iliyopita. Ni matokeo ya usimamizi mbaya kabisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa tatizo hili tata. Jumuiya ya kimataifa pia ina sehemu yake ya lawama kwa kutojali kabisa chanzo cha tatizo na kuruhusu wahusika kufanya kazi nje ya mamlaka yao." Alisema.
Soma pia:Waasi wa M23 waingia Goma
Rais Ruto amesisitiza kuwa mkutano huo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mzozo wa mashariki mwa Kongo utakaofanyika ndani ya muda wa siku mbili zijazo, utajadili namna ya kupanga mikakati ya kusonga mbele ili kulitafutia suluhu suala hilo.
Marais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC wamethibitisha kuwa watahudhuria.