SiasaIran
Marais wa Iran na Urusi wajadili mpango wa nyuklia wa Iran
25 Agosti 2025Matangazo
Rais wa Urusi Vladimir Putin alizungumza kwa njia ya simu na Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, hii ikiwa ni kulingana na Ikulu ya Kremlin na kugusia hali ya mpango wa nyuklia wa Iran.
Ofisi ya rais wa Iran imesema Pezeshkian amemshukuru Putin kwa kuunga mkono "haki ya Tehran ya kurutubisha madini ya urani na kusema Iran "haitafuti na kamwe haitatengeneza silaha za nyuklia.
Iran itafanya mazungumzo na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani mjini Geneva kesho Jumanne baada ya mataifa hayo kutishia kutumia "utaratibu wa kurejesha vikwazo" ambao ni sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, mpaka pale Iran itakubali kudhibiti urutubishaji wa madini ya urani na kurejesha ushirikiano na wakaguzi wa IAEA.