Mapigano yazuka upya Libya
15 Mei 2025Haya ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama. Haya yanafanyika siku moja baada ya mamlaka nchini humo kutangaza kuwa mapigano yamekwisha.
Chanzo hicho cha usalama kimesema kuwa mapigano yameibuka kati ya kundi la Radaa Force na lile la 444 Brigade katika maeneo muhimu mjini humo, ikiwemo katika bandari.
Ripoti za televisheni nchini Libya zinasema mapigano yalipungua mida ya jioni huku baadhi ya maduka yakifunguliwa ila shule zilisalia kufungwa.
Hakuna idadi rasmi ya vifo iliyotolewa ila Shirika la Msalaba Mwekundu la Libya limesema limepata mwili mmoja katika mtaa mmoja huko Tripoli.
Libya imekuwa na wakati mgumu kurudi katika utulivu tangu mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO yaliyomuondoa madarakani Muamar Gadafi.