MigogoroSudan
Mapigano Sudan yaharibu kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta
25 Januari 2025Matangazo
Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF wametupiana lawama kwa kusababisha moto huo. Kiwanda hicho cha al-Jaili kinachopatikana umbali wa takriban kilometa 60 kaskazini mwa mji mkuu Khartoum ni mali ya serikali ya Sudan na kampuni ya mafuta inayomilikiwa pia na serikali ya China, na kina uwezo wa kusafisha mapipa 100,000 ya mafuta kwa siku.
Soma pia: UN: Mzozo nchini Sudan unazidi kuwa mbaya zaidi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea wasiwasi wake kufuatia mapigano yanayozidi makali huko Sudan huku akizitaka pande zote kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuwa na matokeo hatari kwa Sudan na ukanda mzima, ikiwa ni pamoja na athari kubwa za kiuchumi na kimazingira.
-