MigogoroSudan Kusini
Mapigano Sudan Kusini yaua takriban watu 75 tangu Februari
23 Mei 2025Matangazo
Volker Turk ameongezea kwamba makumi ya watu wengine wamejeruhiwa na maelfu kulazimika kukimbia makazi yao katika nchi hiyo.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa zinasema kuwa jeshi la Sudan Kusini lilifanya mashambulizi ya kiholela angani, majini na ardhini dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa SPLA-IO katika Jimbo la Jonglei na Mikoa ya Upper Nile.
Sudan Kusini, ambayo ilipata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka 2011, ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 2013 na 2018 vilivyosababisha vifo vya watu laki nne (400,000) na wengine milioni nne kuyahama makaazi yao. Makubaliano ya kugawana madaraka ya 2018 kati ya pande zinazopigana yaliruhusu utulivu wa hali ya juu.