Mapigano makali yazuka kati ya jeshi la Sudan na RSF
20 Mei 2025Matangazo
Jeshi la Sudan limesema mapigano hayo ni sehemu ya uchokozi mkubwa. Miripuko ilisikika katika eneo hilo, ambako RSF ilirudi nyuma baada ya jeshi la Sudan kuchukua tena udhibiti wa mji mkuu, Khartoum mwezi Machi.
Jeshi limesema operesheni yake ililenga kuwafurumusha wanamgambo hao ambao wamekuwa katika vita tangu Aprili 2023.
Wakati huo huo, mkuu wa jeshi la Sudan ambaye pia ni kiongozi wa nchi hiyo, Jenerali Abdel-Fattah Burhan amemteua waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo tangu ilipotumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka miwili iliyopita.
Kamil al-Taib Idris atakuwa na jukumu la kuunda serikali ya mpito. Waziri Mkuu wa zamani Abdalla Hamdok, alijiuzulu mwaka 2022 wakati wa mkwamo wa kisiasa na maandamano makubwa ya demokrasia.