MigogoroAfrika
Makabiliano makali ya Jeshi na RSF yaripotiwa Sudan
13 Julai 2025Matangazo
Kwa mujibu wa chanzo hicho, jeshi rasmi la Sudan, lilirejesha udhibiti wa maeneo kadhaa muhimu ya mji ambayo RSF waliyateka Ijumaa.
Maeneo hayo ni pamoja na gereza la Shala na makao makuu ya kikosi maalumu cha polisi kinachotoa mafunzo ya kivita.
Hata hivyo chanzo kutoka upande wa wapiganaji wa Rapid Support Forces, RSF kinasema maeneo yote yanayodaiwa kurejeshwa na jeshi, bado yako chini ya udhibiti kamili wa wanamgambo hao likiwemo soko la mifugo la mji huo. Mapigano kote Sudan yamesababisha vifo vya maelfu ya raia tangu yalipoanza Aprili 2023 huku mamilioni ya wengine wakiwa wakimbizi.