Mapigano ya kikabila Ghana yauwa watu 31, yawahamisha 48,000
5 Septemba 2025Matangazo
Maafisa wa serikali walisema Alhamisi, huku zaidi ya watu 13,000 wakikimbilia nchi jirani ya Ivory Coast.Waziri wa Mambo ya Ndani, Mubarak Muntaka, amesema Waghana 13,253 wamevuka mpaka kuingia Ivory Coast, idadi ambayo pia imethibitishwa na afisa wa serikali ya Ivory Coast kwa shirika la habari la AFP. Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Maafa la Ghana (NADMO) liliiambia AFP kuwa takriban watu 48,000 wamelazimika kuondoka makwao kutokana na machafuko hayo, ambayo chanzo chake ni mzozo wa ardhi.