Mapigano katika mkoa wa kusini wa Kandahar nchini Afghanistan
8 Julai 2006Matangazo
Wanamgambo sita wa Taliban wameuwawa kufuatia mapigano yaliyoripuka hivi karibuni nchini Afghanistan.Msemaji wa jeshi la Marekani amesema pia kiwamba wanajeshi kadhaa wa nchi shirika wamejeruhiwa.Mapigano yaliyozuka katika mkoa wa kusini wa Kandahar,yangali yanaendelea katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo.Mnamo wiki za hivi karibuni vikosi vya Marekani zimeanzisha opereshini kadhaa dhidi ya waasi wa Taliban,walioanza upya mashambulio baada ya muda mrefu wa utulivu.