Mapambano makali yaripotiwa katika wilaya ya Kalehe, Kongo
11 Aprili 2025Mashuhuda wanasema mapambano makali yamefanyika tangu mapema asubuhi katika kijiji cha Kasheke baada ya mapambano mengine makali kutokea hapo na katika vijiji vya Lemera, Bushaku na kwenye baadhi ya vijiji vya wilaya za Kabare na Kalehe. Vyanzo vya mashirika ya kiraia vilikadiria kuwa karibu vijiji 12 vimekuwa chini ya udhibiti wa Wazalendo, habari ambayo haijathibitishwa na M23.
Waasi wa M23 nchini waondoka katika mji wa Walikale
Pamoja na kupongeza juhudi za Maimai Wazalendo, Patrick Kubesha , mkazi wa Kivu Kusini amewalaumu kwa mashambulizi yao ya mara kwa mara ambayo husababisha raia wengi kutekwa nyara.
Siku ya Alhamisi, Wazalendo walifanya mashambulizi mengine kando ya Mbuga ya Wanyama ya Kahuzi-Biega kuelekea Tshivanga hadi eneo linaloitwa Kafurumaye, ambapo sio mbali na barabara ya Kitaika namba 3 eneo la Miti-Bunyakiri. Wengine walikwenda kwenye eneo la Murhesa lililopo kati ya vijiji vya Miti na Mudaka.
Kongo na waasi wa M23 kuanza mazungumzo ya ana kwa ana
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Muungano wa AFC unaolijumuisha kundi la M23 umeeleza kukerwa kwake kufuatia kile inachoeleza kuwa ni ukiukaji mkubwa wa hatua ya usitishaji vita pamoja na haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Kinshasa, hasa katika maeneo ya Walikale huko Kivu Kaskazini na Minembwe katika jimbo la Kivu Kusini.
Muungano huo wa AFC/M23umesema umedhamiria kulifanyia kazi suala la amani katika kuutatua mzozo unaoendelea nchini Kongo na inasisitiza dhamira yake ya kulinda na kuutetea umma na kuondoa vitisho vyote.