Rais wa zamani wa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, anayetuhumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaodhibiti eneo la Mashariki mwa Kongo amerejea nchini humo na kwenda kwenye eneo hilo. Je! maana yake ni nini? na hasa baada ya bunge kumvua Kabila, hadhi ya kisheria ya kumkinga dhidi ya mashtaka. Mwenyekiti ni Zainab Aziz