Kwenye kipindi cha Maoni Meza ya Duara, wachambuzi wetu wanaijadili Sudan Kusini. Mkataba wa Amani wa mwaka 2020 uliiimarisha serikali ya mseto ya rais Salva Kiir na makamu wake wa kwanza Riek Machar lakini huo haukuwa mwarobaini kamili kwa sababu nchi hiyo haijawahi kuwa tulivu. Jee! kwa nini Sudan Kusini mara kwa mara inarudi pale pale, kwenye migogoro? Mwenyekiti ni Zainab Aziz