Kipindi cha Krismasi kikiwadia, maduka huwa yanajaa wateja wakiwatafutia wapendwa wao zawadi. Hali hiyo sio tu nchini Ujerumani, bali pia nchi nyingine nyingi za Ulaya. Kuna wanaohoji kwamba lengo la kusherehekea Krismasi limepotea, na badala yake umekuwa wakati wa kununuliana zawadi.