Man United na Tottenham zatinga 16 bora Europa League
31 Januari 2025Timu za Manchester United na Tottenham Hotspur zimejikatia tiketi ya hatua ya 16 bora ya Europa League, baada ya kushinda mechi zao jana Alhamisi, licha ya masaibu zinayokumbana nayo katika Ligi Kuu ya England.
United ilishinda 2-0 dhidi ya FCSB ya Romania, kwa mabao ya Diogo Dalot na Kobbie Mainoo, huku Tottenham ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Elfsborg ya Sweden kupitia mabao ya Dane Scarlett, Damola Ajayi na Mikey Moore.
Soma pia: Leverkusen kutumia maumivu ya Ligi ya Uropa kushinda Pokal
United ilimaliza kundi lake bila kupoteza, ikiwa nyuma ya Lazio na Athletic Bilbao, huku Spurs pia ikisonga mbele.
Lazio, Eintracht Frankfurt, Olympique Lyon, Olympiacos na Rangers ziliepuka mechi za mchujo, huku Roma, Anderlecht, Fenerbahce, Ajax, Galatasaray, Porto na Twente zikifuzu kupitia mechi za kutafuta mshindi.