Man City yaingia mkataba wa pauni bilioni 100 na Puma
16 Julai 2025Kulingana na shirika la habari la PA, makubaliano hayo yatadumu kwa miaka 10 na kila mwaka klabu hiyo itakuwa ikijiwekea kibindoni pauni milioni 100.
Hili ni ongezeko kubwa la thamani ya makubaliano ya kimkakati baina ya klabu ya Manchester City na kampuni hiyo kubwa kabisa ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Puma yaliyofikiwa katika msimu wa 2019-2020.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kuweka kigezo kipya cha mikataba ya kutengeneza jezi kati ya vilabu vya Uingereza na yanapindukia mkataba wa miaka 10 uliofikiwa kati ya klabu ya Manchester United na kampuni ya Adidas wa pauni milioni 900, uliotiwa saini mwaka 2023.
Manchester City imekuwa ikifanya vyema tangu mwaka 2020. Imeshinda mara nne mfululizo ubingwa wa Ligi ya Premier ya England na kuchukua makombe matatu ndani ya msimu mmoja wa2022-23. Hata hivyo hawakuchukua ubingwa mwaka uliopita.
City itaanza kampeni yake ya Ligi ya Premier kwa msimu wa 2025-26, Agosti 16 kwa mechi ya ugenini dhidi ya Wolverhampton Wanderers