JamiiSyria
Mamlaka za Syria zaanzisha uchunguzi wa mauaji ya Sweida
1 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na Shirika la habari la serikali, SANA jana, Wizara ya Sheria ya Syria imesema kamati hiyo itafanya kazi ya kufichua "mazingira yaliyosababisha mashambulizi kwenye jimbo la Sweida," na kuwafikisha wahusika mahakamani. Kamati hiyo itawasilisha ripoti ya mwisho baada ya miezi mitatu.
Mapigano katika jimbo la Sweida mapema mwezi Julai yaliua mamia ya watu, maelfu wakiyakimbia makazi yao, na kutishia kuisambaratisha serikali ya mpito ya baada ya vita nchini Syria.
Kamati kama hiyo iliundwa mwezi Machi, wakati ghasia za kidini zilipozuka Pwani ya Syria na kuua mamia ya raia wa madhehebu ya walio wachache ya Alawite.