JangaMarekani
Mamlaka kuchunguza vifaa kwenye ndege iliyoanguka Marekani
31 Januari 2025Matangazo
Bodi ya Kitaifa inayosimamia Usalama wa Usafirishaji, NTSB, imesema wamevipata vifaa ambavyo hurekodi sauti na taarifa za safari za ndege ya Bombardier CRJ700, iliyogongana na helikopta jana mjini Washington.
Soma pia: Karibu miili ya watu 28 yaopolewa Washington
Msemaji wake, Peter Knudson, amesema vifaa hivyo viko kwenye maabara ya NTSB kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
China imepeleka salamu ya pole kufuatia ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu wote 67 waliokuwemo kwenye ndege hiyo, miongoni mwao ni raia wawili wa taifa hilo.