MigogoroUkraine
Mamia wakusanyika Berlin kuiunga mkono Ukraine
10 Machi 2025Matangazo
Polisi walisema mamia ya watu walihudhuria, lakini waandaaji walikadiria kulikuwa na maelfu ya wahudhuriaji.
Waandamanaji walikusanyika hatua chache kutoka kwa ubalozi wa Marekani, na wa Urusi ambao pia uko karibu na eneo hilo.
Maandamano hayo yaliandaliwa na muungano unaohusisha shirika la kampeni la Campact na chama cha mshikamano cha Ukraine Vitsche na kuhudhiriwa pia na baadhi ya wanasiasa.