Mamia wapinga azma ya NATO kuongeza matumizi ya ulinzi
23 Juni 2025Matangazo
Siku ya Jumapili, wanachama wa NATO walikubaliana kuongeza matumizi yao ya ulinzi hadi asilimia 5 ya Pato la Taifa. Uhispania ilijaribu kuzuia hatua hiyo, lakini kulifikiwa makubaliano ya kutoihusisha na hatua hiyo inayotarajiwa kupitishwa katika mkutano wa Jumanne.
Ikiwa hatua hiyo itapitishwa, mataifa yote wanachama wa NATO isipokuwa Uhispania, yatatakiwa kufikiwa mwaka 2035 kufikia lengo hilo ambalo limekuwa likishinikizwa na rais wa sasa wa Marekani Donald Trump.