Mamia waaandamana Berlin dhidi ya CDU kuhusu uhamiaji
30 Januari 2025Mamia ya watu wameandamana nje ya makao makuu ya chama cha upinzani cha Christian Democrats (CDU) kupinga hatua ya muungano wa vyama vya kihafidhina kushirikiana na chama cha mrengo mkali wa kulia, AfD, kupitisha muswada wa sera ya kudhibiti uhamiaji.
Kulingana na makadirio ya awali ya polisi, takriban watu 650 walihudhuria maandamano hayo, yaliyoandaliwa wakati mswada ukipitishwa bungeni. Maandamano hayo yalipangwa na Amnesty International na mashirika mengine ya haki za kiraia.
Soma pia: Chama cha siasa kali cha AfD chashika nafasi ya pili Ujerumani
Kura hiyo ilizusha mjadala mkali baada ya kiongozi wa CDU, Friedrich Merz, ambaye anatazamiwa kuwa Kansela ajaye, kusema yuko tayari kukubali msaada wa AfD ili mapendekezo hayo yapite.
Vyama vyote vikuu vilisema havitashirikiana na AfD, wakati ambapo Wajerumani wengi wakihofia umaarufu unaoongezeka wa chama hicho katika miaka ya hivi karibuni.