Mamelodi Sundowns yashindwa kuidhibiti Borussia Dortmund
22 Juni 2025Matangazo
Sundowns ya Afrika Kusini walitangulia kufunga bao dakika ya 11 kupitia Lucas Ribeiro, lakini dakika tano baadaye Felix Nmecha alisawazishia Dortmund.
Serhou Guirassy aliipa Dortmund uongozi wa 2-1 dakika ya 34, kisha Jobe Bellingham, aliyeanza mechi hii kwa mara ya kwanza, alifunga bao lake la kwanza tangu alipojiunga na klabu hii ya Ujerumani.
Katika mechi nyengine Bayern Munich walilaza Boca Juniours 2-1, Esperance Sportive wakifunga Los Angeles 1-0 huku Inter Milan ikipata ushindi wa 2-1 didi ya Urawa Red Diamonds.
Hii leo Real Madrid itakipiga na CF Pachuca, Huku Juventus ikitarajia kuchuana na klabu ya Moroko Wydad.