Malori 120 ya chakula cha msaada yaruhusiwa kuingia Gaza
28 Julai 2025Mamlaka ya Israel inayohusika na Masuala ya Palestina, COGAT kupitia chapisho kwenye mtandao wa X imethibitishwa kuingizwa kwa msaada huo wa chakula katika ukanda wa Gaza.
Wakati huo huo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema madai kuwa nchi yake inatumia njaa katika vita vyake dhidi ya Hamas kwenye ukanda wa Gaza ni ya uongo mkubwa.
Malori 100 ya misaada yaruhusiwa na Israel kuingia Gaza
Netanyahu amesema kuwa sera ya njaa haipo Gaza, na wala hakuna njaa Gaza, huku akisisitiza kuwa katika kipindi chote cha vita, wameruhusu na kuwezesha misaada ya chakula kuingia Gaza.
Israel pia ilitangaza kusitisha kimkakati operesheni za kijeshi katika ukanda wa Gaza na kuahidi kufungua njia salama za misaada, na pia kuyataka mashirika ya misaada kuongeza usambazaji wa chakula.