MigogoroMashariki ya Kati
Malori 100 ya misaada yaruhusiwa na Israel kuingia Gaza
27 Julai 2025Matangazo
Jeshi la Israel limeanza leo hii kutekeleza hatua ya usitishaji mapigano kwa kipindi cha saa 10 kwa siku katika maeneo ya Gaza City, Deir al Balah na Mawasi ili kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo hayo yanayokaliwa na watu wengi.
Mkuu wa ofisi ya masuala ya kiutu na misaada wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher amepongeza hatua ya Israel kuruhusu uwepo wa njia salama kwa misafara ya kibinadamu inayoelekea Gaza , na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utajaribu kadri uwezavyo kuwafikia watu wengi zaidi wanaokabiliwa na njaa.