Malkia Elizabeth wa Pili ziarani Uganda
22 Novemba 2007Matangazo
Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza amepokewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi alipowasili Uganda kwa ziara yake ya kwanza nchini humo tangu mwaka 1954.Malkia Elizabeth amefuatana na mumewe Mwana Mfalme Phillip kwa ziara rasmi ya siku mbili kabla ya kufunguliwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kimataifa.Pakistan ni mada inayotazamiwa kuchukua sehemu kubwa ya majadiliano ya mkutano huo.Pakistan inakabiliwa na kitisho cha kusimamishwa uanachama wake,iwapo Rais Pervez Musharraf hatojiuzulu kama kiongozi wa majeshi na kuondosha pia hali ya hatari aliyotangaza mwanzoni mwa mwezi huu wa Novemba.