Muungano wa AES wavutana na Algeria
7 Aprili 2025Nchi za kanda ya Sahel zilizounda muungano wao wa kijeshi za Mali,Burkina Faso na Niger zimesema zimewaondowa mabalozi wao nchini Algeria kujibu hatua ya kudunguliwa kwa droni ya Mali.
Nchi hizo zimeilaumu Algeria kupitia mitandao ya kijamii kwa kuchukua hatua hiyo dhidi ya Mali na kukiita kitendo hicho kama hatua ya kutowajibika ambayo imekiuka sheria ya kimataifa.Togo yadhihirisha dhamira ya kujiunga na Muungano wa AES
Muungano huo wa AES umesema kitendo cha Algeria kinakwenda kinyume na mahusiano ya kihistoria na maslahi ya pamoja kati ya watu wa shirikisho hilo na watu wa Algeria.Mali, Burkina Faso, Niger zaanzisha ushuru mpya wa pamoja
Akiilalamikia Algeria kupitia taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa wizara ya mambo ya nje, waziri mkuu wa Mali, Abdoulaye Maiga alikanusha madai ya serikali ya mjini Algiers kwamba droni ya Mali iliingia kwenye anga yake bila idhini kwa zaidi ya kilomita 2.