Mali yajiondoa katika nchi zinazozungumza Kifaransa
19 Machi 2025Mali imejiondoa katika muungano wa kimataifa wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, siku chache baada ya majirani zake wawili kuchukua hatua kama hiyo.
Katika barua iliyoonekana na shirika la habari la AP hapo jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali amemuandikia mwenzake wa Ufaransa kwamba serikali ya Mali imeamua kujiondoa kwenye muungano huo uitwao Francophonie, akiituhumu Ufaransa kwa kuiwekea vikwazo na kuudharau uhuru wa Mali.Yafahamu mataifa mengine ya magharibi yenye vikosi vya kijeshi Afrika Magharibi
Siku ya Jumatatu, msemaji wa muungano wa mataifa ya Mali, Niger na Burkinafaso, Oria Vande Weghe, alisema Burkina Faso na Niger tayari zilikuwa zimeamua kujiondoa kwenye Muungano huo wa mataifa yanayozungumza Kifaransa.
Hata hivyo, Muungano huo tayari ulizisimamisha uanachama nchi hizo tatu baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo pia zimevunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa na kuwafukuza wanajeshi wa Ufaransa na kugeukia Urusi badala yake.