Mali, Burkina Faso, Niger zaanzisha ushuru mpya wa pamoja
31 Machi 2025Matangazo
Umoja wa Mataifa ya Sahel ulianza mwaka 2023 kama mkataba wa usalama kati ya watawala wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger, walioingia madarakani kwa mapinduzi miaka michache iliyopita.
Sasa umoja huo una mipango ya kuanzisha paspoti ya pamoja, na mfungamano mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijeshi.
Ushuru huo mpya unaanza kazi mara moja, na utahusu bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nje ya mataifa hayo matatu, ingawa hautajumuisha misaada ya kiutu.