Mali, Burkina Faso na Niger zakataa kujiunga tena na ECOWAS
5 Aprili 2025Matangazo
Katika mahojiano yaliodumu kwa masaa manne, Faye aliviambia vyombo vya habari kwamba aliwaomba viongozi wa mataifa hayo kuja pamoja na kufanya mazungumzo ya kuiimarisha jumuiya hiyo ya kikanda.
Lakini rais huyo wa Senegalameongeza kuwa, kama ilivyo kwa mataifa mengine, nchi hizo nazo ni huru na zina uhuru wa kufanya maamuzi yao.
Maamuzi ya Mali, Burkina Faso na Niger yaheshimiwe
Rais Faye ameongeza kuwa kile kinachohitajika ni kuheshimu maamuzi ya nchi hizo kwa kutambua kwamba amefanya kila kitu kuzirudisha tena kwenye jumuiya hiyo.
Nchi hizo tatu za Sahel zilijiondoa katika Jumuiya yaECOWAS mwanzoni mwa mwaka huu, zikiushutumu umoja huo kwa kuegemea upande wa Ufaransa na kushindwa kuzisaidia katika vita dhidi ya makundi ya itikadi kali.