UchumiMalawi
Malawi yapiga marufuku mauzo ya nje ya madini
13 Februari 2025Matangazo
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ina utajiri mkubwa wa madini, ikiwemo ya urani, rubi na yakuti au sapphire lakini, tofauti na majirani zake, bado haijanufaika kwa kuongezeka faida zake.
Waziri wa Madini Joseph Mkandawire amesema serikali imedhamiria kuisafisha sekta ya madini. Wizara itafanya mageuzi ya kuleta ufanisi na uwazi katika usimamizi wa haki za madini.
Amesema marufuku ya kusaifirisha nje madini inaanza kutekelezwa mara moja na itaendelea kwa muda usiojulikana. Uamuzi huo unafuatia amri ya makamu wa rais wa nchi hiyo ya kuzitathmini kandarasi zote zilizopo, mchakato unaotarajiwa kuchukua siku 21.