Malawi yajiandaa kuondoa wanajeshi kutoka DR Kongo
6 Februari 2025Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), kilichopelekwa mwaka 2023 kusaidia serikali ya Kinshasa kukabiliana na machafuko katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.
"Rais Lazarus Chakwera amemuagiza mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Malawi kuanza maandalizi ya kuondoka... ili kuheshimu tamko la usitishaji mapigano," ofisi yake ilisema Jumatano usiku. Pia, hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa mazungumzo yaliyopangwa kwa ajili ya amani ya kudumu.
Kongo yasema tangazo la M23 la usitishaji mapigano ni "mawasiliano ya uongo"
Haijabainika lini wanajeshi hao wataanza kuondoka. Kikosi cha SADC kinachoongozwa na Afrika Kusini kinakadiriwa kuwa na takriban wanajeshi 1,300, huku Tanzania pia ikichangia wanajeshi.