SiasaUturuki
Maandamano Istanbul ya kumuunga mkono meya aliyefungwa jela
8 Mei 2025Matangazo
Kiongozi huyo amekuwa kinara wa kampeni ya upinzani dhidi ya serikali. Maandamano hayo ya Jumatano yalikuwa moja kati ya makubwa zaidi katika wiki za karibuni na yalijiri wakati chama cha upinzani cha Republican People's - CHP kikijipanga kuanzisha upya juhudi zake kwa ajili ya kuachiwa Imamoglu ambaye alizuiliwa mwezi Machi.
Kiongozi wa CHP Ozgur Ozel aliuambia umati huo kuwa mapambano yao ni ya kudai demokrasia na uhuru.
Imamoglu, ambaye alikamatwa Machi 19 kwa mashitaka ya ufisadi ambayo anakanusha vikali, anaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa kiongozi wa muda mrefu Recep Tayipp Erdogan. Kukamatwa kwake kunaweza kumzuia Imamoglu kushiriki uchaguzi wa rais unaopangwa 2028.